mwalimu
• 1418 Videos
Favorites
441 Views
Description
Tangu Siku Hiyo Aliponijia
- Tangu siku hiyo aliponijia
- Akae moyoni mwangu,
- Sina giza tena, ila mwanga pia,
- Kwa Yesu Mwokozi wangu
- Amani moyoni mwangu,
- Kwa Yesu, Mwokozi wangu,
- Sina shaka kamwe, Kwa sababu Yeye,
- Yu nami moyoni mwangu
- Sina haja tena ya kutanga-tanga,
- Ndiye Kiongozi wangu.
- Dhambi zangu zote zimeondolewa,
- Na Yesu, Mwanawe Mungu
- Amani moyoni mwangu,
- Kwa Yesu, Mwokozi wangu,
- Sina shaka kamwe, kwa sababu Yeye,
- Yu nami moyoni mwangu
- Matumaini yangu ni ya hakika,
- Katika Mwokozi wangu.
- Hofu zangu na hamu zimeondoka,
- Kwa kuwa ninaye Yesu
- Amani moyoni mwangu,
- Kwa Yesu, Mwokozi wangu,
- Sina shaka kamwe, kwa sababu Yeye,
- Yu nami moyoni mwangu
- Siogopi tena nikiitwa kufa,
- Yu nami daima, Yesu.
- Mlango wa Mbinguni ni Yeye pia,
- “Tapita humo kwa damu”
- Amani moyoni mwangu,
- Kwa Yesu, Mwokozi wangu,
- Sina shaka kamwe, kwa sababu Yeye,
- Yu nami moyoni mwangu
- Nitaketi na Yeye huko milele,
- Nisifu Mwokozi wangu.
- Nina raha moyoni majira yote,
- Kwa Yesu, Mwanawe Mungu
- Amani moyoni mwangu,
- Kwa Yesu, Mwokozi wangu,
- Sina shaka kamwe, kwa sababu Yeye,
- Yu nami moyoni mwangu
User Reviews
Be the first to write a review