Kazi Yangu Ikisha
“When My Life Work Is Ended”
1. Kazi yangu ikisha, nami nikiokoka;
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua mwokozi nifikapo ng’amboni;
Atakuwa wa kwanza kunilaki.
Nitamjua, Nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, Nitamjua, kwa alama za misumari.
2. Furaha nitapata nikiona makao;
Bwana aliyotuandalia,
Nitamsifu Mwokozi kwa rehama na pendo;
Vilivyonipa pahali mbinguni.
Nitamjua, Nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, Nitamjua, kwa alama za misumari.
3. Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
Nitamjua, Nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, Nitamjua, kwa alama za misumari.
4. Milangoni mwa mji Bwana atanipisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele, lakini;
Nataka kumwona mwokozi kwanza.
Nitamjua, Nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, Nitamjua, kwa alama za misumari.